Askofu
Cletus Chandrasiri Perera, mwakilishi wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Sri Lanka anasema, maadhimisho ya Kongamano la 51 la Ekaristi Takatifu
Kimataifa Jimbo kuu la Cebu, Ufilippini ni fursa ya kuadhimisha,
kuabudu, kutafakari na kuzama katika katekesi za kina zinazotolewa
wakati huu wa kongamano, ili kuwawezesha waamini kuonja na hatimaye,
kushuhudia utajiri mkubwa unaofumbatwa katika Fumbo la Ekaristi
Takatifu, kiini na kilele cha maisha na utume wa Kanisa.
Maadhimisho ya Kongamano la 51 la Ekaristi Takatifu kimataifa yanajikita katika Ibada ya Misa takatifu,Sala, Katekesi, Tafakari, Ibada ya Kuabudu na Maandamano la Ekaristi Takatifu ushuhuda wa imani ya Kanisa katika Fumbo la Ekaristi Takatifu, kielelezo cha uwepo endelevu wa Kristo kati ya waja wake pamoja na mikutano mbali mbali ya kiimani. Inafurahisha kuona kwamba, Baba Mtakatifu Francisko ameridhia maadhimisho ya Kongamano hili yafanyike nchini Ufilippini, nchi ambayo ina idadi kubwa ya waamini wa Kanisa Katoliki, watu ambao wako moto moto katika ushuhuda wa imani yao kwa Kristo na Kanisa lake, ikilinganishwa na nchi nyingine kutoka Barani Asia.
Maadhimisho haya ni mkusanyiko wa waamini kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanaoshuhudia umoja na utofauti wao katika imani na upendo. Wote hawa wanaungana kwa pamoja ili kumwomba Kristo Yesu awaongoze na kuwaimarisha katika imani inayoshuhudiwa katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili. Ekaristi takatifu ni kiini na hitimisho la maisha na utume wa Kanisa, kama ambavyo wanakaza kusema Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican.
Maadhimisho haya ni
wakati muafaka kwa Wakristo kutoka Sri Lanka waliohamia nchini
Ufilippini kuweza kukutana na kusali kwa pamoja, ili kushuhudia imani
yao katika Fumbo la Ekaristi Takatifu anasema Askofu Cletus Chadrasiri
Perera, mwakilishi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Sri Lanka kwenye
maadhimisho ya Kongamano la 51 la Ekaristi Takatifu Kimataifa
linaloendelea huko Jimbo kuu la Cebu, Ufilippini.
Habari kwa hisani ya Radio Vaticani
If you're looking to burn fat then you have to start using this totally brand new tailor-made keto meal plan diet.
ReplyDeleteTo design this keto diet, licensed nutritionists, personal trainers, and top chefs joined together to develop keto meal plans that are powerful, suitable, money-efficient, and delicious.
Since their grand opening in January 2019, 100's of clients have already remodeled their body and health with the benefits a professional keto meal plan diet can give.
Speaking of benefits; clicking this link, you'll discover eight scientifically-confirmed ones provided by the keto meal plan diet.