Lengo kuu ya jumuiya yetu ni kumtangaza Bwana YESU aliye alfa na omega katika historia ya wokovu wa binadamu wote hapa duniani.
Pages
- Home
- MALENGO YA JUMUIYA
- NGUVU YA ROZARI TAKATIFU
- PICHA ZA BWANA YESU
- AMRI ZA MUNGU
- AMRI ZA KANISA
- MFUMO WA UONGOZI
- SALA YA ASUBUHI
- SALA YA JIONI
- SALA MBALI MBALI
- MASOMO YA JUMAPILI NA TAFAKARI
- UMUHIMU WA SKAPULARI
- MAPAJI SABA YA ROHO MTAKATIFU
- KATEKISIMU KATOLIKI
- UFASIRI WA BIBLIA KATIKA KANISA
- “ROZARI YA BIKIRA MARIA”
- NANI MWABUDU SANAMU ?
- CONTACT US
- PICHA ZA BIKIRA MARIA
- HISTORIA NA UKUU WA BIKIRA MARIA
Thursday, January 16, 2014
Angola kwa mara ya kwanza inatarajia kuadhimisha Siku ya Vijana Kitaifa 2015
Baraza la Maaskofu Katoliki Angola, linatarajia kunako Mwaka 2015 kuadhimisha kwa mara ya kwanza Siku ya Vijana Kitaifa. Lengo ni kuhakikisha kwamba, vijana kutoka nchini Angola wanapewa nafasi ya kuweza kushirikisha karama na vipaji vyao kwa ajili ya ujenzi, ustawi na maendeleo ya Kanisa na Taifa katika ujumla wake. Hayo yamejadiliwa hivi karibuni katika Bunge la Vijana wa Angola.
Askofu Zeferino Martins, Mwenyekiti wa Tume ya Vijana ya Baraza la Maaskofu Katoliki Angola anasema, vijana wengi nchini humo wanakabiliwa na tatizo la ulevi wa kupindukia, hali ambayo inabomoa misingi bora ya maisha ya kikristo na kiutu, kiasi hata cha kudhohofisha maisha ya ndoa na familia. Baraza la Maaskofu Katoliki Angola linasema, kuna haja kwa wadau mbali mbali kuwekeza katika majiundo makini ya vijana, ili kudhibiti tabia ya ulevi ambayo inawatumbukiza vijana hata katika majanga mengine ya maisha.
Maaskofu wanasema, umefika wakati kwa Angola kutoa kipaumbele cha kwanza katika maisha na utume wa Familia. Changamoto hii inakwenda sanjari na maandalizi ya Maadhimisho ya Sinodi maalum ya Maaskofu kuhusu Familia itakayoadhimishwa mjini Vatican mwezi Oktoba, 2014.
Habari : Radio vatican
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment