Thursday, January 16, 2014

Askofu mwandamizi Tsegaye Keneni ateuliwa kuwa Askofu wa Vikarieti ya Kitume ya Soddo, Ethiopia



Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi la kung'atuka kutoka madarakani lililotolewa na Askofu Rodrigo Meija Saldarriaga wa Vikarieti ya Kitume ya Soddo, nchini Ethiopia kadiri ya sheria za Kanisa Namba 401, Ibara 1.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu mwandamizi Tsegaye Keneni Derra kutoka Vikarieti ya Soddo, kuwa Askofu wa Vikarieti ya Kitume ya Soddo, kuanzia tarehe 12 Januari 2014. 


Habari : Radio vatican

No comments:

Post a Comment