Friday, October 31, 2014

Papa ataja wajumbe wapya washauri kwa Shirika la utajaji Watakatifu

Baba Mtakatifu amemteua wajumbe wapya washauri kwa ajili ya Shirika la Utajaji Wenye Heri na Watakatifu. Nao ni Padre Bernard Ardura, O. Praem, Rais wa Kamati ya Kipapa ya Sayansi Historia.; Monsinyori Cifres Alejandro Gimenez, Mkutubu katika Shirika kwa ajili ya Mafundisho ya Imani; Padre Paulo Carlotti, SDB, Mkurugenzi Katika Mahakama ya Kitume ya Kitubio, Padre Tomislav Mrkonjić, O.F.M. . Mtalaam katika hati za maandishi ya mkono ; Padre Paulo Murray, OP, Rais wa Taasisi ya Kiroho katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thomas Aquinas, Padre Martin McKeever, C.SS.R., Rais wa Alphonsian; Jordi Pique Augusti P. Collado, OSB, Rais wa Taasisi ya Kipapa ya Liturujia katika Taasisi ya Kipapa ya Anselm Athenaeum; Padre Rocco P. Ronzani, Osa, Makamu Mkuu katika Taasisi ya "Augustinianum"; Padre Pablo Santiago Zambruno, OP, Profesa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thomas Aquinas; Padre Raffaele Di Muro, O.F.M. . Conv​​, Profesa katika Kitivo cha Kipapa Theolojia cha Mtakatifu Bonaventure; Wengine ni Prof. Gabriele Zaccagnini, Profesa katika Chuo Kikuu cha Pisa, Prof. Angela Ales Bello, Mjumbe wa kawaida katika taasisi ya Kipapa Taaluma ya Teolojia.

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment