Papa
katika homilia yake, Jumanne 7Oktoba katika Kanisa dogo la Mtakatifu
Marta alitafakari somo la waraka wa Mtakatifu Paulo kwamba, Bwana
alichagua watu wake na kuwasindikiza kipindi chote cha maisha yao ya
nyikani. Mtakatifu Paulo anakumbuka maisha yake ya dhambi, na mambo
ambayo Mungu aliyatenda kwa watu wake. Mtakatifu Paulo hafichi dhambi
zake , alizofanya yeye mwenyewe. Na hata sisi tunapaswa kukumbuka kwamba
tumetenda dhambi, alisema Papa.
"Sisi tulichaguliwa. Ni neema kubwa ambayo tuliipata, ni neema ya upendo", Papa aliendelea kutafakari na kusema kufanya kumbukumbu ni kuuona ukweli wa hali hiyo , kwani Paulo anaungama ni jinsi gani alivyo vuruga Kanisa , na hasemi "mimi nilikuwa mwema , mimi nilikuwa mtoto wa yule, au mwenye kuwa na uwezo", hapana , Paulo alisema "mimi nilikuwa mtesaji na mtu mbaya", aliikumbuka safari yake ya maisha.
Papa alibainisha kwamba Kufanya kumbukumbu ya namna hii katika maisha yetu kwa wengi ni nadra, wengi tunasahau mambo tunayoyaishi muda huo huo, na si vyema kusahau ya nyuma, kama ilivyo kila mmoja wetu ana historia, historia ya neema, historia ya dhambi, historia katika safari ya maisha, historia ya mambo mengi. Papa alieleza na kuhimimiza kwamba, ni muhimu kusali kwa ajili ya historia, Paulo alifanya hivyo akielezea kidogo historia yake na kwa ujumla anasema kwamba Yeye alinichaguliwa, Yeye aliitwa, yeye aliokolewa, yeye alisindikizwa katika safari ya maisha.
Kufanya kumbukumbu ya safari yako mwenyewe ni kutangaza utukufu wa Mungu aliendelea Papa, kukumbuka dhambi zetu ambazo Bwana Mungu alituokoa,ni kuupa utukufu wa Mungu. Mtakatifu Paulo anasema alimwokoa kwa mambo mawili dhambi zake na neema ya Mungu msulibiwa.
Paulo alikuwa akifanya kumbukumbu yake na kujisifu , nimekuwa mkosefu, lakini Kristo msulibiwa ameniokoa, na hivyo kufanya kitendo hicho ilikuwa ni kujisifu, na hii ndiyo kumbukumbu ya Paulo ambayo hata sisi tumeitwa kuifanya.
Aidha Papa alirejea somo la Injili ambamo Yesu anamwambia Marta, unahangaika kwa mambo mengi , lakini kuna jambo moja tu, Maria amechagua nafasi iliyo bora.
Ni nini maana yake, Papa aliuliza, ni kumsikiliza Bwana na kufanyakumbukumbu, haiwezekani kusali kila siku kama vile sisi hatuna historia, kila mmoja anayo ya kwake, na katika historia hiyo ndiyo tunayo wakilisha katika sala kama alivyofanya Maria. Lakini wakati mwingine tumejazwa mahangaiko kama ya Marta, kazi za kila siku ,katika kufanya kile ambacho tunapaswa kufanya, kinasasababisha kusahau historia hii.
Uhusiano wetu na Mungu, Papa aliongeza hauanzi siku ya kubatizwa , unaaza tangu Bwana alipotuangalia na kutuchagua , Ni katika moyo wa Mungu uhusiano unaanza, wa kufanya kumbukumbu ya uchaguzi wetu ,ule unaotokana na utashi wa Mungu juu yetu. Kumbukumbu ya safari yetu ya muungano. Je Muungano huo unaheshimiwa? Aliuliza.
Sisi ni wadhambi na tunapaswa kufanya kumbukumbu , kufanya kumbumbu ya Mungu asiye katisha tamaa,na yeye ndiye tumaini letu. Na hii ndiyo sala ya kweli Papa alimalizia homelia yake akiwaomba wote kusali zaburi ya 138.
E Bwana umenichunguza na kunijua. Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;umelifahamu wazo langu tokea zamani ,Umepepeta kwenda kwangu na kulaĆa kwangu.
Hii ndiyo sala Papa alisema kusali ni kufanya kumbukumbu mbele ya Mungu katika historia yetu, Kwa sababu historia yetu, ni historia ya upendo juu yetu.

Habari kwa hisani ya radio vatican
No comments:
Post a Comment