Baba
Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 22 Oktoba 2014 kabla ya Katekesi
yake kwa wageni na mahujaji kutoka sehemu mbali mbali za dunia,
alikutana na kuzungumza na wachezaji wa timu ya mpira F.C. Bayen Munich
kutoka Ujerumani baada ya mashindano kati yake na timu ya A.S. Roma
iliyochabangwa magoli 7- 1, jambo ambalo liliwasikitisha sana mashabiki
wa timu ya Roma.
Viongozi wa Timu ya Bayen Munich walimzawadia Baba Mtakatifu mpira ambao ulikuwa una majina ya wachezaji wote wa timu ya Bayen Munich pamoja na kumpatia Jezi maalum iliyoandikwa kwa lugha ya kijerumani, "Franziskus". Timu hii ya Mpira itamzawaidia Baba Mtakatifu Francisko kiasi cha Euro Millioni moja katika mashindano mbali mbali ya kirafiki yatakayofanywa na Timu hii katika kipindi cha mwaka mzima.
Baba Mtakatifu ataitumia fedha hii kwa ajili ya kuwasaidia maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii.

Habari kwa hisani ya radio vatican
No comments:
Post a Comment