Tuesday, October 14, 2014

Wito na utume wa Familia katika Kanisa na Ulimwengu mamboleo! Kauli mbiu kwa Sinodi ya Maaskofu kwa Mwaka 2015



Baba Mtakatifu Francisko ametangaza kwamba, maadhimisho ya awamu ya pili ya Sinodi ya Maaskofu kuhusu familia yatafanyika kuanzia tarehe 4 hadi tarehe 25 Oktoba 2015 mjini Vatican, yakiongozwa na kauli mbiu "Wito na Utume wa Familia katika Kanisa na Ulimwengu mamboleo". Taarifa hii imetolewa na Kardinali Lorenzo Baldiseri, Jumatatu tarehe 13 Oktoba 2014 wakati wa Kikao cha kumi na nne cha Sinodi maalum ya Maaskofu kuhusu familia.

Mababa wa Sinodi wanaendelea na majadiliano kuhusu matatizo, changamoto na fursa zilizopo katika familia, huku wakiongozwa na dhana ya ukweli, uwazi na kwamba, Mababa wengi wa Sinodi wanaendelea kushirikisha uzoefu na mang'amuzi yao kuhusiana na familia. Maadhimisho ya Sinodi, ambao ni muda maalum kwa Kanisa kutembea kwa pamoja katika sala na tafakari yanahudhuriwa kwa sehemu kubwa na Baba Mtakatifu Francisko. 

Habari kwa hisani ya radio vatican

No comments:

Post a Comment